Keeping up with Boi: Scamming

Boi is playing games on his Fathers phone. The Phone pings, its an SMS message.

“Dad! Dad! uko na message kwa simu.”  Said Boi while handing the phone to the Dad. 

“Ebu nione, imetoka kwa nani.” Said Baba Boi.

‘H11S1UKWEL1 Confirmed. You have received Ksh5,000.00 from JEFF MPORAJI on 28/06/2022 at 12:11 PM. New balance is KshXXX.’ 

Read the message.

“Hii message si yangu, hakuna pesa nimepata kwa simu.” He said. “Wacha niangalie balance ya account yangu.”

“Umepata pesa Baba Boi?” asked Mama Boi, elated.

Shortly afterward the phone rings before he responds to Mama Boi.

“Hallo, Kwa majina naitwa Jira kutoka Safari Telcom Customer Care, napiga kukuarifu kwamba kuna customer ametuma pesa kwa bahati mbaya na tungependa uweze kumrudhishia.” Said the person on the phone.

“Sawa, kwa hivyo unataka nifanye aje ili kurudisha pesa yake.” Asked Baba Boi.

“Ningependa kuomba tafadhali utupatie nambari yako ya kitambulisho pamoja na nambari yako ya siri ili tuweze kufanya transaction kutoka upande wetu.” Asked the person on the phone.

“Nipatie dakika mmoja niweze kuangalia balance yangu ya pesa kwa simu.” Said Baba Boi. “Kwa sababu sijaona balance yangu imebakia ngapi.”

“Ni sawa.” Replied the person.

“Naona ni kama balance yangu imebakia vile ilikuwa hapo kitambo.” Said Baba Boi.

“Balance imebakia pesa ngapi?” asked the person.

Baba Boi is starting to get suspicious.

“Kama uko kwa customer care unaweza kuona balance yangu.” He said. “Uko sure unapiga kutoka Safari Telcom?”  he asked.

“Wewe nipatie nambari ya siri ili niweze kurudishia mteja pesa yake.” Said Jira.

“Kata simu Baba Boi! Kata simu saizi!” instructed Mama Boi. “Huyo mtu ni mkora, hafanyi kazi na Safari Telcom.”

“Ni kama…” Said Baba Boi

“Kwani hujaona anakuitisha password yako alafu ajaribu kukuibia pesa.” Said Mama Boi. “Ni bahati nzuri hakuna kitu umeweza kumwambia.”

“Angalia message nilipata.” Said Baba Boi as he was handing the phone to Mama Boi. 

“Hii message haijatoka kwa Safari Telcom.” Said Mama Boi. “Angalia, ni message imetumwa na number ya kawaida.”

“Eeeeh, karibu atuibie pesa!” Said Baba Boi.

“Sijui kama unakumbukua ule kijana kutoka kwa Flash Squad?” Said Mama Boi. “Alikuwa anaitishwa PIN number yake ndio waweze kumwekea pesa yenye ameshinda kwa simu.”

“Next time ukipata message kama hizo, usifungue, usionyeshe watu na pia usiforward kwa mtu mwingine.” Said Mama Boi.  “Hao ni wakora.”